Marehem, Aisha Mainda enzi za uhai wake. |
Bada ya danadana nyingi, hatimaye mwili wa mnenguaji Aisha Madinda unafanyiwa upasuaji muda huu katika hospitali ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao Saluti5, mkurugenzi wa Aset Asha Baraka amebainisha kuwa upasuaji umeanza dakika 10 zilizopita na ni zoezi linalotarajiwa kuchukua masaa mawili.
Asha Baraka amesema baada ya zoezi hilo, mwili wa marehemu utaandaliwa kwa maziko.
Mazishi ya Aisha Madinda yatafanyika Kigamboni makaburi ya Kibada leo mchana muda wowote baada ya sala ya Ijumaa.
USIPITWE NA HII: CHAMELEON APELEKA KILIO KWA WEMA!!!!
USIPITWE NA HII: CHAMELEON APELEKA KILIO KWA WEMA!!!!
0 Response to "MWILI WA MAREHEMU AISHA MADINDA WAFANYIWA UCHUNGUZI...TAARIFA HAPA..."
Post a Comment