ZA UKWELI SANA

MHE.JOSHUA NASSAR KIZMBANI KWA TUHUMA ZA UTEKAJI......SOMA ZAIDII



   

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha Mhe. Joshua Nassari.
Na Woinde Shizza, Arusha
MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha Mhe. Joshua Nassari  anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kutuhumiwa na tukio la kumteka mtendaji wa kata ya makiba.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas alisema kuwa Mhe Nassari  huyu alikamatwa majira ya saa moja usiku  December 16 katika eneo la Doli lililopo  katika kijiji cha UsaRiver  kwenye gari aina ya Land cruiser  lenye namba za usajili T 753 AQR.
Alisema kuwa mbunge huyo anatuhumiwa kumteka mtendaji kata aliyefahamika kwa jina la Nemani Ndundu  wa kata ya Makiba tarafa ya Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha  December 15  majira ya saa mbili asubuhi katika eneo la Maji ya Chai.
Kamanda Sabas amesema  mtendaji huyo alikumbwa na tukio hilo wakati alipokuwa katika pikipiki yake akielekea kwenye kata ambapo inatuhumiwa kuwa Mh. Nassari alimkamata na kumpiga na kumjeruhi katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtaka amuonyeshe majina ya wanachama waliopiga kura katika kituo cha  huduma na maendeleo kilichopo katika kata yake.

Kamanda Sabas alisema kuwa  mpaka sasa Mhe Joshua Nassari anashikiliwa na polisi na anatarajiwa kufikisha mahakamani  ya wilaya ya Arumeru leo December 17 kujibu tuhuma zinazomkabili.

0 Response to "MHE.JOSHUA NASSAR KIZMBANI KWA TUHUMA ZA UTEKAJI......SOMA ZAIDII"

Post a Comment