ZA UKWELI SANA

ANUSURIKA KUUAWA KATIKA WIZI WA PIKIPIKI MAGOMENI, DAR!!!

Mtuhumiwa wa wizi akiwa amechakazwa kwa kipigo
KIJANA ambaye jina lake haikufahamika mara moja, amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kwa tuhuma za wizi wa pikipiki jijini Dar.Tukio hilo la kusisimua limetokea asubuhi ya leo Magomeni-Mwembechai,  ambapo lilisababisha foleni ndefu ya  magari wakati kijana huyo akiadhibiwa na wananchi.
Pamoja na kipigo alichopewa, wananchi waliamua kumvisha tairi shingoni wakiwa tayari kumchoma moto ambapo dakika chache tu baadaye askari walifika na kumwokoa.
Kijana huyo aliyekuwa bado hai, aliokolewa na askari  wa doria waliomchukua pamoja na mtu aliyejitaja kama mmiliki wa pikipiki iliyoibiwa.

source GPL.

0 Response to "ANUSURIKA KUUAWA KATIKA WIZI WA PIKIPIKI MAGOMENI, DAR!!!"

Post a Comment