ZA UKWELI SANA

BREAKING NEWS!!!! MWANAMUZIKI MKONGWE, SHEM IBRAHIM KARENGA HATUNAYE TENA!!!

Shem Ibrahim Karenga enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI mkongwe mwenye umahiri wa kuimba na kucharaza gitaa kiongozi la Solo, Shem Ibrahim Karenga amefariki dunia leo akiwa katika Hospitali ya Amana  jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.

Wengi wanamfahamu Shem Karenga kupitia tungo zake mbalimbali zilizochangia kumpa umarufu, alizozifyatua akiwa na bendi hizi na zile, kama vile ‘Tucheze Segere’, ‘Muna’, ‘Kila jambo’ na ‘Mbelaombe’.

Mpaka mauti yanamfika, Shem Karenga Mkurugenzi Msaidizi katika Bendi ya Tabora Jazz Star ambapo Mkurugenzi Mkuu ni Ibrahim Didi.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Shem Karenga anatarajiwa kuzikwa kesho. RIP!

0 Response to "BREAKING NEWS!!!! MWANAMUZIKI MKONGWE, SHEM IBRAHIM KARENGA HATUNAYE TENA!!!"

Post a Comment